Jina takatifu la Yesu


Jina takatifu la Yesu (kwa Kiebrania יֵשׁוּעַ, Yēšū́aʿ, Yeshua'; yaani "YHWH anaokoa", hivyo "Mungu Mwokozi") ni namna jina la Yesu linavyotajwa na wafuasi wake kwa heshima kubwa zaidi ya Mungu Baba.

Kifupisho IHS juu ya altare kuu ya Kanisa la Yesu, Roma. Kifupisho hicho kinatumika pia juu ya mavazi na vifaa vya ibada.[1] Kilitokana na jina lake kwa Kigiriki ΙΗΣΟΥΣ, si katika maneno ya Kilatini Iesus Hominum Salvator, yaani Yesu Mwokozi wa Binadamu, kama ilivyosemekana.
IHS, Montmorency, Ufaransa
Math 1:18-21 katika nakala ya karne ya 11.
IHS, malaika na taji la miba, Hostýn, Ucheki.

Historia

hariri

Katika Kanisa Katoliki ibada hiyo ilistawi hasa mwishoni mwa karne za kati, sambamba na ile kwa Moyo mtakatifu wa Yesu.

Litania ya Jina Takatifu ilitungwa na Wafransisko wa karne ya 15 (Bernardino wa Siena na Yohane wa Capistrano) walioeneza sana ibada hiyo.[2]

Sikukuu ya Jina Takatifu ilikubaliwa mwaka 1530. Siku hizi inaadhimishwa na Kanisa la Kilatini kama kumbukumbu tarehe 3 Januari[3].

Hata hivyo heshima kwa jina hilo takatifu ilianza na Ukristo wenyewe (taz. Mdo 4:10).[4][1][5] Karne hata karne, Wakristo wamelitumia wakiamini lina uwezo wa pekee sana.[1][6]

Heshima hiyo ilisisitizwa na Mtume Paulo kwa ajili ya wokovu (Fil 2:10; taz. Rom 10:3)[7]. Kwa kuwa yeye alidai kwa jina la Yesu kila goti lipigwe mbinguni, duniani na kuzimu, imekuwa desturi ya wengi walau kuinamisha kichwa katika kulitaja, kama anavyotakiwa kufanya padri wa Kanisa la Kilatini wakati wa Misa.

Ibada ya namna hiyo ipo katika Ukristo wa mashariki pia (k.mf. Sala ya Yesu).[8] Vilevile madhehebu mbalimbali yanaadhimisha sikukuu hiyo kwa jina lilelile la Wakatoliki au kama Tohara ya Yesu, kwa kuwa ndipo alipopatiwa jina, siku ya nane baada ya kuzaliwa.

Tanbihi

hariri
  1. 1.0 1.1 1.2 Gieben, Servus. Christian sacrament and devotion 1997 ISBN 90-04-06247-5 p.18
  2. Catholic encyclopedia: Litany of the Holy Name
  3. Martyrologium Romanum
  4. Hunter, Sylvester. Outlines of dogmatic theology, Volume 2 2010 ISBN 1-146-98633-5 p.443
  5. Becker, Udo. The Continuum encyclopedia of symbols 2000 ISBN 0-8264-1221-1 p.54
  6. Strecker, Georg and Horn, Friedrich Wilhelm Horn. Theology of the New Testament 2000 ISBN 0-664-22336-2 .p89
  7. Tuckett, Christopher Mark. Christology and the New Testament 2001 ISBN 0-664-22431-8 pp.58-59
  8. Houlden, Leslie. Jesus: the complete guide 2006 ISBN 0-8264-8011-X p.426

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Jina takatifu la Yesu kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.