Jaipur
Jaipur ni mji mkuu wa jimbo la Rajastan nchini Uhindi. Mnamo mwaka wa 2011, karibu watu milioni tatu waliishi hapo. Iko mnamo km 300 kusini magharibi kwa Delhi na takriban km 200 magharibi kwa Agra.
Kuna viwanda mbalimbali katika jiji hilo, ambalo pia ni kitovu cha kiutamaduni kinachopokea watalii wengi.
Paoneaanga pa kale pa Jantar Mantar, kitovu cha kihistoria cha Jaipur na Ngome ya Amer vimepokewa katika orodha ya Urithi wa Dunia ya UNESCO. Jaipur ina chuo kikuu.
Ni pia kitovu cha usafiri ambako njia za reli na barabara muhimu zinakutana.
Ni mmoja kati ya miji ya Uhindi ambako uhaba wa maji ya kunywa ni mkali; kufuatana na makadirio maji yanaweza kwisha kabisa mnamo mwaka 2020.[1]
Vyanzo
hariri- ↑ India has just five years to solve its water crisis, experts fear. Otherwise hundreds of millions of lives will be in danger, taarifa ya CNN ya July 4, 2019
Tovuti nyingine
hariri- media kuhusu Jaipur pa Wikimedia Commons
Makala hii kuhusu maeneo ya Uhindi bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Jaipur kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |