Hiroshima ndio mji mkuu wa Mkoa wa Hiroshima.

Hiroshima

Bendera
Nchi Japani
Kanda Chūgoku
Mkoa Hiroshima
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 1,169,018
Tovuti:  www.city.hiroshima.jp
Jengo la "Kuba ya Bomu la nyuklia" ni ghofu la nyumba linalohifadhiwa kama kumbukumbu ya mlipuko wa mwaka 1945.

Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2009, mji huo una wakazi wapatao milioni 1.2.

Uko kwenye kisiwa cha Honshu.

Mji umekuwa maarufu sana duniani kwa sababu ulikuwa mji wa kwanza katika historia kushambuliwa kwa bomu la nyuklia. Tarehe 6 Agosti 1945 ndege ya kivita ya Marekani ilitupa bomu moja lililoua watu 75,000 mara moja na takriban 60,000 wengine walikufa baadaye kutokana na mnururisho wa kinyuklia. Wengine waliendelea kufa kwa sababu ya kansa iliyosababishwa na mnururisho.

Mji ukajengwa upya baada ya vita kuu ya pili ya dunia. Jengo la "Kuba ya Bomu ya nyuklia" ni ghofu la nyumba linalohifadhiwa kama kumbukumbu ya mlipuko. Imeingizwa katika orodha ya urithi wa dunia.

Tovuti za nje

hariri
  Makala hii kuhusu maeneo ya Japani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Hiroshima kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.