Herufi
Herufi ni alama katika mwandiko unaofuata alfabeti. Kila herufi ni alama ya sauti au fonimu fulani kama vile A - B - C. . Kifinisia na Kigiriki zilikuwa lugha za kwanza zinazojulikana zilitumia mtindo huu.
Alfabeti ya Kilatini (kwa matumizi ya Kiswahili) | ||||||
---|---|---|---|---|---|---|
Aa | Bb | Cc | ch | Dd | ||
Ee | Ff | Gg | Hh | Ii | Jj | |
Kk | Ll | Mm | Nn | Oo | Pp | |
Rr | Ss | Tt | Uu | Vv | ||
Ww | Xx | Yy | Zz |
Miandiko iliyotangulia muundo huu ilikuwa na alama moja kwa silabi moja yaani mwandiko wa silabi.
Muundo mwingine tena ni alama moja kwa neno moja jinsi ilivyo hadi leo katika Kichina. Faida ya herufi za alfabeti ni ya kwamba alama chache zinatosha kwa kuandika lugha yote. Katika mwandiko wa Kichina mwanafunzi anahitaji kujifunza alama mamia kabla hajaanza kuandika kitu.
Herufi zinazotumiwa zaidi duniani ni zile za alfabeti ya Kilatini. Alfabeti nyingine zinazotumiwa kimataifa ni hasa alfabeti ya Kiarabu na alfabeti ya Kikirili. Herufi zao zatofautiana kwa jumla ingawa kuna pia herufi zinazofanana katika kundi la alfabeti. Kwa mfano alfabeti za Kilatini na Kikirili zote zimetokana na alfabeti ya Kigiriki.
Vilevile alfabeti ya Kiarabu ina herufi za nyongeza ikitumiwa kwa kuandika lugha kama Kiajemi, Kiurdu au lugha za Kiturki.