Babu wa Kanisa ni jina la heshima ambalo kuanzia karne IV Kanisa Katoliki limewapatia Wakristo wa kale (hadi mwaka 750 hivi), wenye utakatifu, elimu na imani sahihi, ambao mafundisho yao yanawezesha kujua mapokeo ya Mitume.

Mababu wa Kanisa, mchoro mdogo wa karne ya 11 kutoka Kiev, Ukraina.

Orodha ya kwanza ya mababu wa Kanisa iliandikwa katika Hati ya Gelasio (karne VI); baadhi yao waliongezewa jina la Mwalimu wa Kanisa.

Muhimu zaidi upande wa Mashariki ni: Atanasi, Basili Mkuu, Gregori wa Nazienzi na Yohane Krisostomo.

Upande wa Magharibi ni: Ambrosi, Agostino wa Hippo, Jeromu na Papa Gregori I.

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Babu wa Kanisa kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.